Mapigano Sudan Kusini yawalazimisha maelfu kukimbilia CAR,Uganda na DR Congo

Mapigano Sudan Kusini yawalazimisha maelfu kukimbilia CAR,Uganda na DR Congo

Mapigano katika maeneo ambayo awali yalikuwa na utulivu kwenye jimbo la Equatoria Magharibi Sudan Kusini yanaendelea kuwafungisha virago maelfu ya watu na kukimbilia katika nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Uganda n ahata Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatumai kupata fursa ya kuwafikia wakimbizi wa Sudan Kusini 7000 juma lijalo ambao wako katika hali mbaya kwenye eneo ambalo ni vigumu kufikia la Bambouti Mashariki mwa CAR. Msafara wa UNHCR na WFP wa chakula na vifaa vingine unatarajiwa kuondoka Bangui kesho Jumamosi kwenda Bambouti.

Watu wengine 11,000 wamekimbilia DR Congo kwenye jimbo la Haut Eele wakati Uganda wameingia Zaidi ya watu 14,000 kwenye makazi ya Adjumani wilaya ya Nile Magharibi na wachache kwenye kambi za Arua na Kiryandongo. Wengi wa wakimbizi wote ni wanawake na watoto. Leo Dobbs ni msemaji wa UNHCR..

(SAUTI YA LEO DOBBS)

"Wakimbizi wapya wanaowasili Bambouti wamezidi kiasi cha wakazi wa mji huo na wanakandamiza kwa kiasi kikubwa rasilimali za asili za jamii, katika sehemu ambayo tayari kuna shida ya kliniki za afya, shule moja tu katika sehemu hiyo ambayo pia ilifungwa mwaka 2002, afya nayo ni shida, kuna magonjwa ya Malaria, kuhara, Utapiamlo na vipele."