Barubaru na wanawake ndio walio katika hatari zaidi kwenye vita dhidi ya HIV na Ukimwi

Barubaru na wanawake ndio walio katika hatari zaidi kwenye vita dhidi ya HIV na Ukimwi

Lengo la kimataifa la kutokomeza HIV na ukimwi ifikapo mwaka 2030 litafanikiwa tuu endapo unyanyapaa utakabiliwa sanjari na vita hivyo. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

(Taarifa ya Grace)

Huo ni mtazamo wa Kate Gilmore, naibu kamishina wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa, alipohutubia baraza la haki za binadamu mjini Geneva Ijumaa.

Ameonya kwamba ubaguzi umewaacha walio wachache katika hatari licha ya vita dhidi ya ukimwi na HIV kupewa msukumo mkubwa katika malengo ya maendeleo ya milenia MDG’s yaliyomalizika 2015.

Bi Gilmore anaainisha hatari hiyo hususani kwa vijana barubaru

(SAUTI YA KATE GILMORE)

Kimataifa babarubaru ndio kundi la umri ambao vifo vya ukimwi vimeongezeka katika muda wa MDG’s, ongezeko la karibu asilimia 50, wakati kila kundi la umri mwingine limekuwa na punguzo la asimilia 32 au zaidi katika wakati huohuo.”

Ameongeza kuwa changamoto nyingine ni kuendelea kwa ubaguzi dhidi ya wanawake ambao wanakataliwa huduma za afya zinazostahili. Ametoa wito wa fursa kwa wote za dawa za kuokoa maisha ambazo nyingi zina gharama kubwa.