Skip to main content

Onyo la utapiamlo kwa watoto wakati unyanyasaji ukiibuliwa Sudan Kusini:UNICEF

Onyo la utapiamlo kwa watoto wakati unyanyasaji ukiibuliwa Sudan Kusini:UNICEF

Umoja wa Mataifa umesema maelfu ya watoto wako katika hatari Sudan kusini kutokana na vita vinavyoendelea na ukosefu wa fedha muhimu za ufadhili.

Onyo hilo linafuatia kuchapishwa kwa ripoti ya Umoja wa mataifa Ijumaa ikiainisha unyanyasaji mkubwa uliotekelezwa na serikali.

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema mapigano yanaghubika maeneo ambayo awali yalikuwa na amani na kuwaweka watoto pabaya zaidi.

Hivi sasa watoto zaidi ya 160,000 wenye utapiamlo wanahitaji msaada.

Licha ya ombi la dola milioni 155 kusaidia watoto zaidi ya milioni tano ni dola milioni 27 tu zilizopatikana. Christophe Boulierac ni msemaji wa UNICEF

(SAUTI YA BOULIERAC)

 Kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mzozo watoto wako katika tisho kubwa, sio tuu kwa kukosa fursa au uwezo lakini kwa kukosa fedha”