Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yajinasibu kuhusu takwimu kwenye ajenda 2030

Tanzania yajinasibu kuhusu takwimu kwenye ajenda 2030

Mkutano wa 47 wa kamisheni ya takwimu ya Umoja wa Mataifa ukifikia ukingoni leo, Tanzania imesema imeshaandaa mpango wa ufuatiliaji wa masuala ya takwimu kwenye utekelezaji wa ajenda 2030 iliyopitishwa mwaka jana.

Akihojiwa na Idhaa hii kando ya mkutano huo uliopitisha viashiria vya kitakwimu vya kufuatilia malengo 17 ya ajenda hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Taifa ya takwimu nchini Tanzania Dkt. Albina Chuwa amesema mara baada ya kupitishwa kwa ajenda hiyo, waliitisha kikao cha wadau wanaozalisha na kutumia takwimu ili kuelezea mwelekeo unaotakiwa na sasa..

(Sauti ya Dkt. Chuwa-1)

Na kuhusu takwimu na mabadiliko ya tabianchi kwa mujibu wa ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa iliyowasilishwa kwenye mkutano huo Dokta Chuwa amesema..

(Sauti ya Dkt. Chuwa-2)