Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon asihi Iran kutochochea mivutano

Ban Ki-moon asihi Iran kutochochea mivutano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameisihi Iran kutumia umakini katika shughuli zake za kijeshi ili kutoongeza mivutano ya kisiasa kwenye ukanda wa Mashariki ya Kati.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, Katibu Mkuu amekumbusha kwamba vizuizi dhidi ya Iran vimeondolewa na Baraza la Usalama lakini hata hviyo Baraza hilo limeiomba Iran kujizuia na shughuli yoyote ya majaribio ya kutuma makombora yanayoweza kubeba silaha za nyuklia.

Bwana Ban amesema hayo baada ya ripoti za Iran kutuma kombora la ballistika.

Katibu Mkuu ameziomba pande zote zijizuie kuchukua hatua yoyote itakayoweza kuchochea mivutano kwenye ukanda huo, wakati ambapo tayari mazingiria ya kisiasa si tulivu.