Skip to main content

UNICEF yaokoa wanawake wajazito Karamoja, Uganda

UNICEF yaokoa wanawake wajazito Karamoja, Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), kwa ushirikiano na Shirika la Usaidizi wa Kimataifa la Korea, limetoa msaada wa magari matatu ya wagonjwa kwenye eneo la Karamoja, nchini Uganda.

Taarifa ya UNICEF Uganda imeeleza kwamba mradi huo utawasaidia wanawake wajawazito kupata huduma za kuokoa maisha.

UNICEF imeeleza kwamba wanawake wanachelewa kupata huduma za afya ya uzazi katika ngazi tatu: ya kwanza, wakiwa nyumbani , UNICEF ikishauri wanaume kusindikiza wake zao kuona daktari wakati wa ujauzito ili kupata uelewa zaidi.

Tatizo la pili, UNICEF imesema, ni kwa ngazi ya jamii, huku miundombinu hafifu, ukosefu wa usafiri na nyenzo za mawasiliano zikizuia wanawake kupata huduma hizo kwa wakati mwafaka. Sanjari na magari ya wagonjwa, UNICEF inatarajia kuwapatia wanawake vocha za usafiri.

Hatimaye, ucheleweshaji pia hutokea hospitalini ambapo bado vifaa havitoshi na wauguzi wanahitaji mafunzo zaidi.

Mradi wa UNICEF wenye thamani ya dola zaidi ya milioni 8 unalega kusaidia wanawake wenye ujauzito zaidi ya 100,000, pamoja na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano 100,000 kwenye mkoa wa Karamoja.