Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSCA yachukua hatua kudhibiti ghasia kwenye kambi

MINUSCA yachukua hatua kudhibiti ghasia kwenye kambi

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA umechukua hatua thabiti ili kudhibiti mashambulizi ya waasi dhidi ya kambi za wakimbizi na wakimbizi wa ndani kwenye eneo la Bambari nchini humo.

Hatua hizo ni pamoja na kusambaza vikosi vya walinda amani wa Mauritania na Gabon karibu na kambi hizo na tayari wameweza kuzuia shambulio dhidi ya kambi ya wakimbizi wa Sudan Kusini.

Msemaji wa MINUSCA Vladimir Monteiro amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Bangui akiongeza..

(Sauti ya Monteiro)

Miongoni mwa harakati zilizofikiriwa kuchukuliwa na MINUSCA ni kusambaza polisi wa Umoja wa Mataifa kuchunguza ndani ya kambi za wakimbizi wa ndani na kushughulikia suala la risasi na silaha. Ripoti zinaonyesha kwamba risasi na silaha zinakuwepo ndani ya kambi na hii ni hatari kwa usalama wa raia.”

MINUSCA imesema mashambulizi dhidi ya kambi za wakimbizi yalitokea siku chache zilizopita na kusababisha vifo kadhaa.