Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa UM Mashariki ya kati alaani mashambulizi ya kigaidi Israel

Mratibu wa UM Mashariki ya kati alaani mashambulizi ya kigaidi Israel

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa mashariki ya kati, Nickolay Mladenov amelaani mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi huko Israel yaliyosababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 14 wamejeruhiwa.

Katika taarifa yake ya leo, Mladenov amesema mashambuilo hayo yalifanyika katika miji ya Tel Aviv- Jaffa, Petah Tiqva na Yerusalem.

Bwana Mladenov amesema kamwe vitendo vya kigaidi haviwezi kuhalalishwa kwa misingi yoyote ile na kulaani kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitukuza matukio hayo.

Ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa, kidini na kijamii kutoka pande zote kusimama kidete dhidi ya ghasia na uchochezi.