Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwekeza katika wanawake na wasichana ni muhimu kwa mustakhbali bora- UNFPA

Kuwekeza katika wanawake na wasichana ni muhimu kwa mustakhbali bora- UNFPA

Wakati kongamano la Kamisheni kuhusu hali ya wanawake likianza wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu (UNFPA), limesema kuwa kuwekeza katika wanawake na wasichana na kuwawezesha kuna umuhimu mkubwa katika kufikia mustakhbali bora.

Kauli mbiu ya kongamano la mwaka huu ni kuwezesha wanawake na mchango wake muhimu katika kufikia maendeleo endelevu.

Wakati wa kongamano hilo, UNFPA itaandaa mikutano kadhaa kusisitiza umuhimu wa kuwekeza katika wanawake na vijana, hususan wasichana, ikimulika uhakikishaji huduma na haki za afya ya uzazi kwa wote, na kutokomeza aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.