Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa UM watoa mwongozo wa kulinda haki za binadamu wakati wa maandamano

Wataalam wa UM watoa mwongozo wa kulinda haki za binadamu wakati wa maandamano

Wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa wametoa leo ripoti mpya kwa Baraza la Haki za Binadamu, wakieleza kwa upana mapendekezo kwa serikali na vikosi vya polisi duniani kuhusu jinsi ya kudhibiti vyema zaidi mikusanyiko ya hadharani, ili mikusanyiko kama hiyo ichangie kulinda na kufurahia haki za binadamu. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Watalaam hao ambao ni Christof Heyns anayehusika na mauaji holela na Maina Kiai anayehusika na haki ya kufanya mikutano ya amani na kujumuika, wamesema udhibiti mwema wa mikusanyiko unaweza mara nyingi kusaidia kuzuia hali kuzorota na kuibuka ghasia.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ambayo wamesema yanalenga kuwapa wahusika wote mwongozo wa jinsi ya kushulikia mikutano, ni jinsi ya kutoa habari na mipaka ya haki ya kujumuika, wajibu wa serikali katika kuwezesha mikutano, jinsi polisi wanavyopaswa kudhibiti mikutano, ikiwemo matumizi ya nguvu na ufuatiliaji, kurekodi mikutano, upatikanaji wa taarifa, na uwajibikaji.

Sauti ya Kiai)

"Uwezekano wa kuandamana na kuungana pamoja ni muhimu katika maendeleo ya kijamii kama njia ya kutoa mawazo na ni jukumu la kila mwananchi. Maandamano yana mchango mkubwa katika demokrasia ikiwemo katika taasisi zinazoibuka za kidemokrasia na vile vile kuelezea maoni ya kisiasa au uaminifu na taasisi hizo. Kwa mantiki hiyo maandamano hayapaswi kuchukuliwa kama tishio badala yake yachukuliwe kama mazungumzo ambapo mamlaka zinapaswa kushiriki.”