Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japan imeonyesha uungaji mkono mkubwa wa miradi ya UNIDO kwa Afrika:

Japan imeonyesha uungaji mkono mkubwa wa miradi ya UNIDO kwa Afrika:

Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na maendeleo ya viwanda (UNIDO) limesema serikali ya Japan imetoa mchango wa dola zaidi ya milioni 7.4 ili kusaidia mahitaji ya jamii zilizoathirika na matatizo ya kibinadamu na wimbi la wakimbizi wa ndani.

Fedha hizo zitafadhili miradi saba inayoendeshwa na UNIDO barani Afrika na Mashariki ya Kati. Msaada huo wa fedha ulitangazwa mwishoni mwa wiki ililopita kwenye mkutano baina ya mkurugenzi mkuu wa UNIDO LI Yong, na balozi wa kudumu wa Jaopan kwenye shirika hilo Mitsuru Kitano, mjini Vienna, likishuhudiwa na wawakilishi wa Iraq, Jordan, Morocco, na Sudan.

Balozi Kitano amesisitiza uhusiano wa pembe tatu baina ya Japan, UNIDO na nchi zinazopokea msaada , akitumai kwamba mchango huo wa Japan utazinufaisha nchi washirika hususani vijana na wanawake.