Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utekelezaji wa kanuni za kibinadamu Ulaya ujali watoto UNICEF

Utekelezaji wa kanuni za kibinadamu Ulaya ujali watoto UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetaka utekelezaji wa uamuzi kuhusu kanuni za msingi za kibinadamu kupitia mkutano wa Umoja wa Ulaya nchini Uturuki, uongoze mamlaka za Ulaya katika kujali wakimbizi na watoto wahamiaji.

Katika taariaf ya UNICEF kuhusu kanuni hiyo iitwayo usidhuru, shirika hilo limesema wakati haifahamiki vyema namna mpango huo utakavyotekelezwa,  limekumbusha mataifa majukumu kadhaa ikiwamo haki za binadamu katika kudai ulinzi .

Wajibu mwingine ni kwamba watoto hawapaswi kurudishwa  ikiwa wanakabiliana na hatari ikiwamo uwekwaji kizuizini, ajira, usafirishaji haramu au unyanyasaji pamoja na kuruhusu usalama na nia halali kwa watoto katika kukimbia vita na mizozo kwa njia mujarabu ikiwamo kuwaunganisha na famili zao.

UNICEF imesisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watoto hususani wale walio na wazazi  wataepuka madhila ya wasafirishaji haramu wa watu, na wawe salama.

Shirika hilo limesisitiza kuwa hali tete inayojitokeza hivi sasa mpakani mwa Ugiriki na iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia ya Macedonia, haikubaliki kwa watoto ambao ni idadi kubwa ya walioko mpakani Idomeni kaskazini mwa Ugiriki.