Skip to main content

Afya ya uzazi ni haki inayopaswa kuhakikishwa kote duniani: Wataalamu

Afya ya uzazi ni haki inayopaswa kuhakikishwa kote duniani: Wataalamu

Haki ya kupata huduma za afya ya uzazi ni msingi wa kufarijika na haki zingine zote za kibinadamu, wamesema leo wataalam wa Kamati ya haki za kiuchumi, Kijamii na kitamaduni wakikutana huko Geneva, Uswisi.

Wataalam hao waliotoa leo mwongozo wa kisheria wamesema bado mamilioni ya watu, hasa wasichana na wanawake, hawawezi kufurahia haki hiyo, wakikumbwa na vikwazo kadhaa katika kupata huduma za afya ya uzazi, vinavyoathiri haki zao zingine.

Kwa mfano wamesema kupiga marufuku utoaji mimba kwa misingi ya afya na dharura kunaweza kuhatarisha maisha ya mama mjamzito. Wameongeza kwamba maoni ya madaktari hayapaswi kuzuia wanawake kupewa huduma za afya ya uzazi.

Wataalam hao wamezisihi serikali ziwekeze zaidi katika afya ya uzazi ili kupunguza kiwango cha vifo vya wakina mama.