Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imeelezea wasiwasi dhidi ya tamko la wakuu wa nchi wa EU na Uturuki:

UNHCR imeelezea wasiwasi dhidi ya tamko la wakuu wa nchi wa EU na Uturuki:

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limekariri taarifa iliyotolewa na wakuu wa nchi za Muungano wa Ulaya na Uturuki na lina wasiwasi na baadhi ya vipengee vya mapendekezo.

Imesema taarifa hiyo iliyotolewa baada ya mkutano baiana ya EU na Uturuki , UNHCR sio mwanachama wala haina undani wote wa mikakati ya utekelezaji.

Hata hivyo imekaribisha mchango mkubwa wa fedha kutoka kwa Muungano wa Ulaya kuisaidia Uturuki na jumuiya ya wakimbizi nchini humo. Uturuki inahifadhi wakimbizi milioni 3.

Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR William Spindler  wasiwasi wao ni mipango yoyote ya kuwarejesha wakimbizi bila kuzingatia ulinzi wao na pia wajibu wao kimataifa.

(Sauti ya Spindler)

"Tunakaribisha  miradi yote itakayowapa wakimbizi njia halali za kuingia Ulaya kwa idadi ya kuonekana, na kutoka nchi zote jirani, siyo tu wakimbizi wa Syria kutoka Uturuki. Pia ahadi za Muungano wa Ulaya za kuwapa hifadhi ndogo sana zikilinganishwa na mahitaji."