Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS kushirikiana katika teknolojia mpya ya simu ili kuboresha ukusanyaji wa takwimu na kuendeleza vita dhidi ya VVU

UNAIDS kushirikiana katika teknolojia mpya ya simu ili kuboresha ukusanyaji wa takwimu na kuendeleza vita dhidi ya VVU

Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS na kampuni mwendeshaji wa mawasiliano ya simu ya Orange wamesaini mkataba wa maelewano ya kushirikiana katika mradi mpya ili kuimarisha uhusiano kati ya watoa huduma za afya na watu wanaoishi na kuathirika na VVU kupitia njia ya matumizi ya teknolojia ya simu za mkononi.

Teknolojia ya simu za mkononi itatumika kuboresha huduma na kuhakikisha kuendelea kuwepo kwa subira katika uzingajiaji wa huduma na matibabu na kusaidia kukomesha unyanyapaa na ubaguzi.

Takwimu zitakusanywa na kufanyiwa tathimini, mapengo katika huduma yatabainiwa na hatua zitachukuliwa imarisha huduma bora ya afya kwa watu wanaoishi na kuathirika na VVU. Takwimu hizo hazitotaja majina na usiri utahakikishwa.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibé, amesema ili kufikia malengo ya UNAIDS ya “Fast-Track” ifikapo 2020 basi nchi zinahitaji ubunifu. Ameongeza kuwa ushirikiano huu mpya na kampuni ya Orange utazisaidia nchi kunufaika na teknolojia na kuhakikisha zinatoa huduma bota kwa watu wake.

Ushirikiano huo utatumia wavuti maalumu iitwayo M-Tew ambayo itatoa mafunzo na kuwawezesha wahudumu wa afya kuwasiliana na watu waliojiorodhesha kupata huduma kupitia ujumbe wa simu za mkononi, kwa kupigiwa simu au ujumbe wa maneno wa simu za mkononi.