Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuo cha takwimu Mashariki mwa Afrika chatambuliwa kimataifa- Profesa Ngalinda

Chuo cha takwimu Mashariki mwa Afrika chatambuliwa kimataifa- Profesa Ngalinda

Mkutano wa 47 wa kamisheni ya takwimu ya Umoja wa Mataifa unaanza leo New York, Marekani ambapo miongoni mwa mambo yanayojadiliwa ni jinsi takwimu zitasaidia kufanikisha malengo  ya maendeleo endelevu, SDGs.

Miongoni mwa washiriki ni Profesa Innocent Ngalinda mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika ambapo ameiambia Idhaa hii kuwa hatimaye chuo hicho kinatangazwa rasmi kwenye mkutano wa leo kuwa chuo chenye ubora wa kufundishia takwimu rasmi na kitatumia mitaala ya Umoja wa Mataifa, ikimaanisha kwamba..

(Sauti ya Profesa Ngalinda)

Chuo cha Takwimu cha Mashariki mwa Afrika ni chuo pekee barani humo kinachotoa mafunzo ya vitendo kwa watakwimu rasmi na kinaundwa na nchi zote zinazozungumza kiingereza barani Afrika.