Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Iraq wahusishwe zaidi katika maamuzi:UN Women

Wanawake Iraq wahusishwe zaidi katika maamuzi:UN Women

Kitengo cha Umoja wa mataifa kinachohusika na masauala ya wanawake UN Women kwa ushirikiano na kmati ya wanawake ya Bunge nchini Iraq wameandaa mkutano wa ngazi ya juu kwenye baraza la wawakilishi mjini Baghdad ili kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo kimataifa hufanyika kila mwaka Machi 8.

Tukio hilo linakuja katika wakati mgumu ambapo wanawake na wasichana wa Iraq wanaendelea kuwa wahanga wa matukio ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu hasa kuhusiana na ongezeko la ghasia zitokanazo na itikadi kali na watu kutawanyika. Kwa mujibu wa UN Women hakuna mwanamke au msichana aliye huru na hatari ya kutokuwepo na usalma nchini humo, ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo ndoa za lazima , mifumo mingine ya ukatili wa kingono na ukatili wa kijinsia.

Akifungua tukio hilo naibu spika wa baraza la wawakilishi la Iraq Aram Shiekh Mohammad amewapongeza wanawake wa Iraq kwa uongozi shupavu, jukumu lao la kisiasa na kujitolea kwao katika kuunda upya Iraq. Mwakilishi wa UN women nchini humo Hiba Qasas,  ameikumbusha Iraq kuwa mchango wa wanawake ni muhimu hiyo wajumuishwe zaidi katika uongozi na fursa za mamuazi , lakini pia ameitaka serikali kukomesha vitendo vyote vya kibaguzi dhidi ya wanawake na wasichana.