Skip to main content

Wakulima wa Ethiopia wanahitaji msaada wa haraka kulisha taifa lililoghubikwa na ukame:FAO

Wakulima wa Ethiopia wanahitaji msaada wa haraka kulisha taifa lililoghubikwa na ukame:FAO

Wakulima nchini Ethiopia wakati unawatupa mkono kuweza kulisha taifa ambalo kwa sasa linaghubikwa na ukame mkubwa. Grace Kaneiya na ripoti kamili

(TAARIFA YA GRACE)

Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO, mahitaji ya kibinadamu nchini humo yameongezeka mara tatu wakati moja ya msimu mbaya kuwahi kutokea wa El Nino ukiendelea kuliathiri taifa hilo la pembe ya Afrika na kuyaweka njia panda maisha ya wakulima na wafugaji.

Pierre Vauthier ni kiongozi wa timu ya FAO ya kukabiliana na dhoruba nchini Ethiopia anaelezea zaidi kuhusu hali nchini humo

(SAUTI YA PIERRE VAUTHIER)

"Tunachoshuhudia ni kwamba mahitaji  yanaongezeka 2016. Tunachoshuhudia pia baada ya mazungmzo na wadau na serikali ni kwamba msaada wa chakula hauwezi kutegemewa milele, na hivyo tunataka kushughulikia mahitaji ya chakula au sivyo gharama ya kukabiliana na hali hii itaendelea kuongezeka."

Ameongeza kuwa watu takribani milioni 10.2 sasa wanauhaba wa chakula huku robo ya wilaya zote nchini humo zimeelezwa kuwa matatizo ya chakula na janga la utapia mlo. FAO inahitaji dola milioni 13 ifikapo mwisho wa mwezi huu ili kuwasaidia watu zaidi ya 600,000 walioathirika.