Ban akutana na waziri wa mambo ya nje wa Mauritania Isselkou Ould Ahmed Izid Bih:

Ban akutana na waziri wa mambo ya nje wa Mauritania Isselkou Ould Ahmed Izid Bih:

Leo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Mauritania Isselkou Ould Ahmed Izid Bih. Katika mkutano wao Ban ameipongeza serikali ya Mauritania kwa kuunga mkono juhudi zinaoongozwa na Umoja wa mataifa katika kusaka suluhu ya mzozo wa Sahara Magharibi.

Pia ameipongeza nchi hiyo kwa jukumu lake la kuchagiza ushirikiano wa Amani ya kikanda Sahel. Lakini pia amesisitiza haja ya kuzichagiza pande kinzani Mali kusonga mbele na kutekeleza mkataba wa Amani.

Ban pia amemshukuru waziri huyo kwa mchango wa Mauritania kwa mpango wa kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa na kwa sera zake za kutovumilia unyanyasaji wa kingono kwa walinda Amani.