Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ustawi wa wanawake Burundi yamulikwa kuelekea siku ya wanawake

Ustawi wa wanawake Burundi yamulikwa kuelekea siku ya wanawake

Wiki ijayo Jumanne Machi Nane ni Siku ya Wanawake Duniani. Kauli mbiu ya maadhimisho mwaka huu ni “Sayari ya 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2030: Imarisha Juhudi za Kufikia Usawa wa Jinsia”. Maadhimisho ya siku hiyo katika Umoja wa Mataifa yatamulika jinsi ya kuongeza kasi na kuimarisha nguvu ya kutekeleza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women, limesema maadhimisho hayo pia yatamulika ahadi zilizowekwa chini ya mkakati wake wa “Step it UP” au “Imarisha Juhudi”, pamoja na dhamira nyingine kuhusu usawa wa jinsia, kuwezesha wanawake, na kulinda haki za binadamu za wanawake.

Afrika Mashariki, Burundi ni moja ya nchi zinazojivunia kuongeza usawa wa jinsia, hasa katika uwanja wa siasa baada ya kuwapa kwa uchache uwakilishi wa asilimia 30 kwenye taasisi za uongozi wa taifa.

Hata hivo changamoto kubwa ni kumstaawisha mwaaamke wa Kijijini  na yule mwenye kipato cha chini ambao wamezongwa na umaskini, kama anavyosimulia Mwandishi wetu Ramadhani KIBUGA katika Makala hii kutoka Bujumbura.