Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia waendelea kukumbwa na madhila Yemen

Raia waendelea kukumbwa na madhila Yemen

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHRC imesema takribani raia 168 wameuwawa na wengine 193 kujeruhiwa, theluthi tatu ya matukio hayo yakitokana na mashambulizi ya anga mwezi Februari.

Ofisi hiyo imesema kuwa miundombinu ya raia imeendelea kuharibiwa mwezi Februari kutokana na mshambulizi ya pande zote kinzani kuelekezwa katika maeneo ya raia

Rupert Colvile ni msemaji wa ofisi ya haki za binadmau ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI RUPERT)

‘‘Kwa ujumla tangu tarehe 26 mwezi Machi mwaka jana, tuliandikisha raia 3081 waliouwawa nawengine 5733 walijeruhiwa. Idadi hii haijumuishi wahanga wapiganaji, bali ni raia pekee.’’