Shauri la FBI dhidi ya Apple lina madhara kwa uhuru wa watu duniani: Zeid

Shauri la FBI dhidi ya Apple lina madhara kwa uhuru wa watu duniani: Zeid

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amesema shauri la kisheria la  wapelelezi  Marekani FBI dhidi ya kampuni ya tekenolijia ya komputa na simuza mikononi Apple kuweka hadharani  taarifa za simu zake ni hatari kwa uhuru wa watu duniani . Joseph Msami na maelezo kamili.

(TAARIFA YA MSAMI)

Katika taarifa yake leo kuhusu sakata hilo, ameonya kuwa ikiwa majaji watakubaliana na pendekezo hilo la FBI, hatua hiyo ina madhara kwa usaslama wa kimwili na kifedha kwa mamilioni ya watu.

Zeid amwesema licha ya kwamba mchakato wa kesi hiyo unaonekana utachukua muda mrefukufikia umauzi lakini ni muhimu pande husika zikazingatia shauri hilo .

Kamishana Mkuu huyo wa haki za biandmu katika UM amesema kwamba ikiwa mahakama itaamua kuipa ushindi FBI itaashiria kuwa nivigumu kwa Apple au kampuni yoyote ya kimataiaf kuhusu musuala  ya teknolojia kulinda faragha ya wateja wao popote duniani.