Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati mvutano unaendelea wakimbizi wa Burundi wafika 250,000:UNHCR

Wakati mvutano unaendelea wakimbizi wa Burundi wafika 250,000:UNHCR

Watu zaidi ya 250,000 kutoka Burundi sasa ni wakimbizi kutokana na machafuko yanayoendelea na sintofahamu iliyoghubika taifa hilo la Afrika ya Mashariki. Flora Nducha na taarifa kamili.

 (TAARIFA YA FLORA)

Likitangaza hali halisi siku ya Ijumaa, shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi kama anavyofafanua msemaji wa shirika hilo Melisa Fleming

(SAUTI YA MELISA FLEMING)

 “Mvutano nchini Burundi bado ni mkubwa na bado unawafungisha watu virago, tunahofia kwamba idadi hiyo ya watu itaendelea kuongezeka, kunaweza kuwa hakuna mapigano lakini laki kuna hali ya hofu nchini humo”

 Ameongeza kuwa wanaoikimbilia nchi jirani wanaarufu kuhusu ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu Burundi unaohusiana na uchaguzi uliokuwa na utata uliompa ridhaa ya kutawala awamu ya tatu Rais Pierre Nkurunziza.

Hadi kufikia leo ombi la fedha za msaada kwa ajili ya Burundi zemefadhiliwa kwa asilimia tatu tuu.