Skip to main content

Tanzania na Ethiopia zashuhudia ongezeko la wabunge wanawake- IPU

Tanzania na Ethiopia zashuhudia ongezeko la wabunge wanawake- IPU

Ushiriki wa wanawake katika mabunge duniani kote umeshuhudia hali ya kusuasua inayotia wasiwasi , imesema ripoti ya muungano wa mabunge duniani, IPU.

Ripoti imesema idadi ya wanawake wabunge mwaka 2015 iliongezeka kwa asilimia 0.5 tu , ambayo ni karibu asilimia 23 ya viti vyote vya bunge vilivyopo.

Mkurugenzi wa mipango IPU Kareen Jabre, amesema maeneo husika ni pamoja na .…

(Sauti ya Kareen)

“Barani Afrika tumeona ongezeko kwenye ushiriki wa wanawake kwenye siasa, mathalani Ethiopia na Tanzania ikihusishwa na viti maalum na pia motisha mfano Ethiopia ambako vyama vyenye wagombea wanawake vinapatiwa fedha za ziada kwa ajili ya kampeni.”

Amesema iwapo kiwango cha ongezeko la wanawake wabunge kitakuwa kwa kasi hiyo ndogo, malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s yanayohusu usawa wa kijinsia hayatofikiwa mwaka 2030 kama ilivyopangwa.