Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam huru ziarani Burundi kusaka ukweli

Wataalam huru ziarani Burundi kusaka ukweli

Wajumbe wa tume ya wataalam huru wa haki za binadamu waliotumwa na Baraza la haki za binadamu wako ziarani Burundi kwa ajili ya kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu unaoshukiwa kutekelezwa nchini humo.

Akihojiwa na Redio ya Umoja wa Mataifa, mmoja wa wataalamu hao watatu, Maya Sahli Fadel, ambaye ni mratibu maalum wa Muungano wa Afrika kuhusu wakimbizi, na wahamiaji amesema watazingatia usawa na uwazi na kwamba watakutana na pande mbali mbali ikiwemo serikali, jamii na vyama vya upinzani.

(Sauti ya bi Sahli Fadel)

Tuko hapa kwa ajili ya kusikiliza pande zote kinzani na kuelewa zaidi mzozo ulioikumba Burundi. Tunachosubiria kutoka kwa mamlaka za serikali ni kuweza kuwasaidia kupata ukweli kuhusu baadhi ya madai ya ukiukaji wa haki za binadamu.”

Wataalam hao watakuwepo nchini humo kwa siku nane wanatakiwa kuwasilisha ripoti yao ya awali tarehe 21, Machi mbele ya Baraza la Haki za Binadamu.