Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 3 bado waghubikwa na mgogoro nchini Ukraine:UM

Watu milioni 3 bado waghubikwa na mgogoro nchini Ukraine:UM

Watu walioghubikwa na mgogoro nchini Ukarine wanajihisi kutelekezwa wakati hofu ikiendelea kutanda kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ambao umeripotiwa kuhusisha mauaji na utesaji imesema ripoti ya Umoja wa mataifa Alhamisi.

Zaidi ya raia milioni tatu wanaishi kwenye maeneo ya vita mwashariki mwa nchi hiyo ambako silaha nzitonzito na vifaru vimesheheni mitaani na mkataba wa Minsk wa kusitisha mapigano bado uko njia panda kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa.

Hali hususani kwenye eneo la Crimea inatia wasiwasi amesema afisa wa ofisi ya haki za binadamu Gianni Magazzeni akitoa mfano wa hatua mpya ya kuwabagua walio wachache ikiwemo Watatar.

(GIANNI MAGAZZENI)

Ni hali ambayo inasikitisha sana na ambayo inahitaji kuangaziwa na kujadiliwa ni kwa jinsi gani itaweza kutatuliwa siku za usoni. Haya yote ni miongoni mwa majadiliano na mashauriano ya Minsk”