Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya wanawake uchukuliwe kama uhalifu wa utesaji- wataalam wa UM

Ukatili dhidi ya wanawake uchukuliwe kama uhalifu wa utesaji- wataalam wa UM

Wataalam wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, wameonya kuhusu tabia ya kupuuza ukatili dhidi ya wanawake kama uhalifu wa kijinsia na kutotilia uzito madhara yake makubwa dhidi ya wanawake kote duniani.

Onyo hilo limekuja siku chache kabla ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ambayo itaadhimishwa Jumanne tarehe 8 Machi.

Wataalam hao wametoa wito kwa serikali ziuzingatie uhalifu wa kijinsia kama unavyozingatiwa uhalifu wa utesaji, na kuzikumbusha kuwa zinapopuuza wajibu wao wa kupinga, kuzuia au kushughulikia ukatili unaotendwa dhidi ya wanawake na wasichana, zinakuwa zimeunga mkono utesaji na vitendo vingine vya kinyama.

Wamesema uhalifu wa ukatili dhidi ya wanawake hutokana na kuenea kwa udhalilishaji wa wanawake kitamaduni, ambao unahalalisha vitendo hivyo kama sehemu ya mila, utamaduni au dini.