Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kusaidia Burkina Faso kusonga mbele- Ban

UM kusaidia Burkina Faso kusonga mbele- Ban

Umoja wa Mataifa umesema utaisaida mpango wa taifa wa maendeleo wa Burkina Faso ambao serikali itawasilisha wiki ijayo. Joshua Mmali na ripoti kamili.

(Taarifa ya Joshua)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa kauli hiyo leo kwenye mji mkuu Ouagadougou wakati akizungumza na waandishi wa habari, mkutano ambao umehudhuriwa pia na Rais Roch Marc Christian Kaboréa.

Ban amesema usaidizi huo ni muhimu kwani nchi hiyo iko kwenye mwelekeo wa marekebisho na kusaka ustawi baada ya ghasia zilizoikumba mwaka 2014 na 2015 huku akiwapongeza kwa uchaguzi uliofanyika kwa amani na usalama.

Halikadhalika amezungumzia usalama na ustawi wa kibinadamu kwenye ukanda wa Sahel, wakati Umoja wa Mataifa ukiandaa kongamano la kiutu mwezi Mei huko Uturiki..

(Sauti ya Ban)

“Rais na mimi sote tunaamini kuwa wakati wa kushughulikia masuala ya usalama, nchi za Sahel lazima ziangazie chanzo cha ukosefu wa utulivu, umaskini, ukosefu wa ajira, kuenguliwa, ubaguzi na ukwepaji sheria."