Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu milioni 9 wanahitaji msaada katika maeneo yaliyoathiriwa na Boko Haram:OCHA

Watu milioni 9 wanahitaji msaada katika maeneo yaliyoathiriwa na Boko Haram:OCHA

Nchi ya Nigeria na bonde la ziwa Chad yanaendelea kushuhudia machafuko, watu kutawanywa na upungufu wa chakula imesema ripoti ya tathimini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibindamu na Misaada ya Dharura(OCHA).

Imeongeza kuwa ghasia zinazosababishwa na kundi la Boko Haramu na operesheni za kijeshi dhidi ya kundi hilo vinaendelea kusabababisha watu kukimbia nchini Cameroon kwenye jimbo la Kaskazini la Far, jimbo la Lac la Chad, jimbo la Diffa la Niger na Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

OCHA inasema mpango maalumu wa kukabiliana na masuala ya kibinadamu wa mwaka 2016 kwa nchi za Cameroon, Chad, Niger na Nigeria umekamilia, ambapo watu takribani milioni 9.2 kati ya jumla ya watu milioni 20.1 wanaoishi katika maeneo hayo yaliyoathiriwa na Boko Haram wanahitaji msaada wa kibinadamu, ikiwemo malazi, chakula na ulinzi.