Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa makazi, wa kulaumiwa ni serikali- Mtaalamu

Ukosefu wa makazi, wa kulaumiwa ni serikali- Mtaalamu

Hali ya watu kukosa makazi ni tatizo linalokabili nchi zote duniani bila kujali kiwango cha maendeleo au mifumo ya uongozi na ni jambo linaloendelea kuenea bila wanaosababisha hali hiyo kukumbwa na mkono wa sheria. Assumpta Massoi na maelezo kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Hiyo ni kwa mujibu wa mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya makazi Leilani Farha katika ripoti yake aliyowasilisha mbele ya baraza la haki za binadamu mjini Geneva, Uswisi.

Bi. Farha amesema ongezeko la idadi ya watu wasio na makazi ni kiashiria cha serikali kushindwa kulinda na kusimamia haki ya makundi yaliyo hatarini zaidi akiongeza kuwa ni matokeo ya serikali kugeuza ardhi kuwa bidhaa badala ya haki ya msingi kwa raia wake.

(Sauti ya Farha)

“Nasihi serikali na jamii ya haki za binadamu kuazimia kutokomeza ukosefu wa makazi ifikapo mwaka 2030 kwa njia inayokidhi vigezo vya haki za binadamu na kwa kuzingatia kipengele namba 11-A cha ajenda 2030. Tuliahidi kuwapatia hifadhi ya kijamii na kuwapatia makazi makundi ya pembezoni na yaliyobinywa.”