Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa wanawake unabadili maisha Guinea-Conakry

Umoja wa wanawake unabadili maisha Guinea-Conakry

Kuelekea siku ya wanawake duniani tarehe Nane mwezi huu wa Machi, Umoja wa Mataifa unapigia chepuo ushirikishaji wa wanawake kwenye utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ukiangazia lengo namba Tano la usawa wa kijinsia.

Lengo hilo linagusia pamoja na  mambo mengine wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi katika ngazi mbali mbali.

Miongoni mwao ni vikundi vya ushirika ambako huko nchini Guinea-Conakry, wanawake katika kijiji kimoja wamebaini kuwa uthabiti wao uko katika umoja wao na hivyo kuunda kikundi cha ushirika kinachopatiwa usaidizi kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-Women. Je nini wamefanya? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.