Skip to main content

Watu bilioni 5.5 wananyimwa dawa za maumivu wanazohitaji: UM

Watu bilioni 5.5 wananyimwa dawa za maumivu wanazohitaji: UM

Watu wengi wanaumwa au kufa kwa maumivu kwa sababu hawana fursa ya kupata dawa mujarabu licha ya wito wa muda mrefu wa kimataifa wa kuwasidia watu hao wamesema Jumatano wataalamu wa afya wa Umoja wa Mataifa. John Kibego na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA KIBEGO)

Ikizilaumu serikali kwa kutochukua hatua dhidi ya mateso yasiyo ya lazima bodi ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti dawa za kulevya (INCB) imesema takribani watu bilioni 5.5 ama hawana kabisa au wana fursa finyu ya kupata dawa wanazohitaji.

Takwimu mpya zinaonyesha kwamba licha ya kuwepo kwa mikataba miwili ya kimataifa inayohusiana na suala hilo kuwepo tangu mwaka 1971 mataifa mengi bado yapo nyuma katika utekelezaji wake kukiwa na tofauti kubwa katika upatikanaji wa dawa husuasani katika nchi zenye uchumi mdogo.

Ikizindua ripoti yake ya kila mwaka bodi hiyo imeongeza kuwa kutokuwepo na fursa ya huduma za dawa ni kinyume na kifungu nambari 25 cha azimio la kimataifa la haki za binadamu, lakini hali hiyo bado inaendelea duniani.

Werner Sipp, ni Rais wa bodi ya kimatifa ya udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya.

(SAUTI WERNER)

‘‘Tunahitaji utekelezaji bora wa kanuni za msingi za mikataba na matamko ya kisiasa. Kanda na mabara mbalimbali yana matatizo na sera tofauti . Mathalani kinachoendelea Amerika Kusini ni tofauti na Asia ya Kati au Afrika ya Kusini.’’