Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya kutathimini uwezekano wa kuondolewa katika urithi wa dunia Mji mkongwe yakamilika

Kazi ya kutathimini uwezekano wa kuondolewa katika urithi wa dunia Mji mkongwe yakamilika

Ujumbe wa maafisa wa tathimini kutoka makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO mjini Paris, Ufaransa umekamilisha tathimini yake kuhusu uwezekano wa kuondolewa katika orodha ya urithi wa dunia ya mji mkongwe  visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa Katibu mtendaji wa tume ya taifa ya UNESCO nchini Tanzania Dk. Moshi Kimizi serikali ya Zanzibar na tume hiyo zimekamilisha kazi ya uwakili kuhakikisha mji mkongwe hauondolewi katika orodha ya urithi wa dunia.

(SAUTI KIMIZI)

Dk. Kimizi amesema ana matumaini kuwa ripoti ya ujumbe wa tathimini inayoratajiwa mwishoni mwa juma itakuwa na majibu chanya.

(SAUTI KIMIZI)