Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mmoja kati ya nane wanaosihi na virusi vya HIV hunyimwa huduma za afya: UNAIDS

Mmoja kati ya nane wanaosihi na virusi vya HIV hunyimwa huduma za afya: UNAIDS

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Ukimwi UNAIDS linasema mmoja kati ya watu wanane wanaoishi na virusi vya  HIV hukataliwa huduma za afya kwasababu za unyanyapaa.

UNAIDS inasema kuwa kando mwa hayo pia kumekuwa na visa ambapo wanawake wajawazito wenye virusi hivyo hulazimishwa kuwa wagumba.

Katika kuadhimisha siku ya kupinga ubaguzi duniani hii leo, Umoja wa Mataifa unataka unataka upatikanaji wa huduma za afya katika misingi ya usawa na heshima kwa makundi ya pembezoni.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa mkuu wa idara ya haki za bianadamu na sheria katika UNAIDS Luisa Cabral anazungumzia ukubwa wa tatizo hilo.

(SAUTI LUISA)

‘Haya ni makadirio ya ukubwa wa tatizo, kuna mifano halisi mathalani shirika moja liitwalo Asia Catalyst ambalo limetoa makadirioa ya nchi sita za Asia  zina kiwango kikubwa cha unyanyapaa na ubaguzi, kwahiyo taarifa mpya zinajitokeza.’’