Skip to main content

Hali ya chakula CAR ni mbaya, FAO yahitaji fedha

Hali ya chakula CAR ni mbaya, FAO yahitaji fedha

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la chakula na kilimo, FAO na lile la mpango wa chakula WFP yanahitaji jumla dola Milioni 172 kukwamua watu zaidi ya Milioni Mbili waliokumbwa na uhaba wa chakula nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Fedha hizo ni muhimu kwani miaka mitatu ya mzozo imesababisha watu kufurushwa makwao na kukwamisha shughuli za kilimo.

FAO na WFP yamesema matokeo yake mavuno ni hafifu, mwelekeo wa masoko umeyumba huku bei za vyakula zikiongezeka kuliko hata kabla ya mzozo, mathalani uzalishaji wa mazao ulikuwa chini ya asilimia 54 ikilinganishwa na kabla ya mzozo.

Alessandro Constatino, afisa wa FAO kutoka kitengo cha ufuatiliaji wa biashara na masoko anasema kile ambacho walifanya mwaka 2015..

(Sauti ya Alessandro)

“FAO ilipatia kaya 170,000 mbegu na pembejeo za kilimo, na WFP wakati huo huo ilisambaza mgao wa chakula ili kuepusha wananchi wanaokumbwa na njaa kula mbegu za mazao.”