Skip to main content

Watoto 60,000 wanakabiliwa na kifo Somalia

Watoto 60,000 wanakabiliwa na kifo Somalia

Takribani watoto 60,000 wanakabiliwa na kifo nchini Somalia kwa sababu ya kukosa msaada , kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu kwenye nchi hiyo ya pembe ya Afrika.

Mtafaruku wa kisiasa, kurejea mara kwa mara kwa ukame na hata mafuriko, inamaanisha kwamba watoto wapatao milioni tano au nusu ya watu wote wa Somalia wanahitaji aina fulani ya msaada.

Umoja wa mataifa unasema, unahitaji dola takribani milioni 900 kwa ajili ya shughuli za msaada, lakini hadi sasa imepokea asilimia mbili tuu ya fedha hizo.

Peter de Clercq ni mratibu wa Umoja wa mataifa wa masuala ya kibinadamu aliyeko Mogadishu Somalia amezungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa akiwa ziarani hapa makao makuu.

(SAUTI CLERCQ)

"Kuna matumaini makubwa Somalia. Somalia siyo nchi isiyo na maana, kwa kweli ni nchi ambayo inaweza kujilisha kwa urahisi mno, kwa mfano kama tukiwekeza kwenye  kilimo cha umwagiliaji maji, ufugaji na uvuvi, ina nafasi nzuri, kwani kuna bandari inayohudumia mikoa, na ina nafasi muhimu ya kiuchumi ikiwa mazingira mazuri ya yatawekwa sawa , nchi hii itaibuka"