UM walaani mashambulio mawili ya bomu Iraq

UM walaani mashambulio mawili ya bomu Iraq

Mashambulio mawili ya mabomu kwenye mji mkuu wa Ira Baghdad, siku ya Jumapili yamelaaniwa vikali na Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya watu 70 wamepoteza maisha katika mashambulizi hayo ambayo yametokea karibu na soko kwenye mji wa Sadr. Kundi la kigaidi la ISIL, ambalo pia hujulikana kama Daesh, limekiri kuhusika na uhalifu huo.

Kufuatia mashumbulizi hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia msemaji wake ameelezea kusitisikitishwa na vitendo hivyo vinavyolenga masoko na sehemu za ibada huku akitaka watekelezaji wa uhalifu huo kuwajibishwa kisheria.

Kwa upande wake Ján Kubiš, mkuu wa mpango wa Umoja wa mataifa nchini Iraq (UNAMI) ameyaelezea mashambulizi hayo ya mabomu kama ni ni shambulio la makusudi na ni kitendo cha uwoga dhidi ya  raia waliokuwa wakiendesha shughuli zao za kila siku kwa amani.

Ameongeza kuwa ISIL wamefanya hivyo kwa nia ya kuchochea ghasia za kidini.