Watafiti kuchunguza yasiyojulikana kuhusu virusi vya Zika na mahitaji

29 Februari 2016

Watafiti mashuhuri kutoka taasisi muhimu za afya watakutana katika Shirika la Afya kanda ya Amerika, PAHO, kuanzia kesho Machi Mosi had Machi Pili, ili kujadili mahitaji muhimu katika kuunda ajenda ya utafiti katika mlipuko wa virusi vya Zika, na athari zake kwa afya.

Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO), imesema watafiti hao wanapanga kutambua upungufu uliopo katika maarifa ya kisayansi kuhuru virusi vya Zika, athari zake kwa binadamu na hatma ya afya ya umma kwa mabara ya Amerika.

Wanatazamia pia kuchunguza mbu anayeambukiza virusi vya Zika, na mbinu zipi za kuzuia mbu huyo aina ya Aedes aegypti zinafanya kazi.

Wataalam hao pia watamulika maelezo ya jumla kuhusu hali ya sasa ya mlipuko wa virusi vya Zika.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud