Baraza la haki lichagize wanachama kutekeleza ajenda ya maendeleo:Lykettoft

29 Februari 2016

Rais wa baraza kuu la Umoja wa mataifa Mogens Lykettoft  ameonya dhidi ya mapungufu makubwa tangu kuundwa kwa Umoja wa Mataifa, yakiwemo baa la njaa, mauaji ya halaiki, na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza kwenye kikao cha 31 cha baraza la haki za binadamu mjini Geneva pia ameliasa baraza hilo kuchagiza nchi wanachama kutekeleza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

(SAUTI YA LYKETTOFT)

“Hakutakuwa na maendeleo endelevu, hakutakuwa na amani ya kudumu endapo haki za watu zikakiukwa na kupuuzwa. Sasa jukumu kubwa la utekelezaji liko mbele yetu. Serikali zimejizatiti nini zinataka kubadilisha na majukwaa ya kimataifa kama baraza la haki za binadamu lazima zifikirie nini yatafanya kusaidia utekelezaji wa jumla na uwajibikaji."

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter