Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwezesha wanawake na kuendeleza usawa kutasaidia wakati wa majanga- CEDAW

Kuwezesha wanawake na kuendeleza usawa kutasaidia wakati wa majanga- CEDAW

Mkurugenzi wa idara ya mikataba katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Ibrahim Salama, amesema ni dhahiri kuwa majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi huathiri wanawake kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko wanaume, na kwamba njia moja ya kushughulikia tatizo hilo ni kuwawezesha wanawake na kuendeleza usawa wa jinsia. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Bwana Salama amesema hayo leo mjini Geneva, wakati wa mjadala wa Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake, CEDAW, ambao umemulika masuala ya jinsia katika kupunguza madhara ya majanga na mabadiliko ya tabianchi.

Mjadala huo wa leo ni hatua ya kwanza katika mchakato wa kufafanua mapendekezo kuhusu suala la jinsia katika kupunguza athari za majanga na mabadiliko ya tabianchi, ambayo yaliafikiwa katika taarifa ya kamati hiyo mnamo 2009.

Kwa upande wake mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva balozi Modest Mero amezungumzia kile kilichowasilishwa katika ripoti kuhusu utokomezaji wa ubaguzi dhidi ya wanawake.

(SAUTI MERO)