Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ateua kundi la West-Eastern Divan kuwa mtetezi wa uelewa wa utamaduni

Ban ateua kundi la West-Eastern Divan kuwa mtetezi wa uelewa wa utamaduni

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameliteua kundi la West-Eastern Divan Orchestra kama mchagizaji wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya uelewa wa utamaduni kimataifa.

Uteuzi huo umefanyika katika hafla maalumu mjini Geneva iliyohudhuriwa na Katibu Mkuu na muungozaji na mpiga piano mashuhuri duniani Daniel Barenboim, ambaye ni mwanzilishi wa kundi hilo na pia balozi wa Amani wa Umoja wa mataifa.

Ban amesema kazi ya kundi hilo ni ushuhuda tosha wa nguvu ya muziki katika kuvunja vikwazo na kuwa daraja miongoni mwa jamii.  Ameongeza kuwa amefurahi kwamba kundi hilo liko tayari kusaidia katika kazi ya Umoja wa mataifa ya kuhakikisha uundaji wa dunia yenye Amani na inayojumuisha wote.

Muungano wa ustaarabu wa Umoja wa Mataifa utalisaidia kundi hilo katika wajibu wake kama mchagizaji wa kimataifa wa kuvumiliana, kuelewana na mshikamano miongoni mwa watu wa tamaduni na dini mbalimbali.