Ban alaani mfululizo wa mashambulizi Yemen

29 Februari 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kusikitishwa kwake na kuendelea kwa mashambulizi ya anga na ardhini nchiniYemern licha ya kutoa wito mara kwa mara wa kukomeshwa uhasama.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Taarifa ya msemaji wa Ban imesema kwa muktadha huo,Katibu Mkuu amelaani vikali shambulio la Februari 27 lililoekezwa katika soko liitwalo Khaleq mjini Sana’a, lililouwa watu 32 na kujeruhi 41.

Amesema idadi hiyo ya vifo ni kubwa zaidi katika shambulio la mara moja tangu Septemba 2015 na kutuma salamu za rambirambi kwa familia na wahanga.

Ban amezikumbusha pande zote kinzani kuheshimu majukumu yao chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu ambazo zinakataza mashambulizi dhidi ya raia ikiwamo masoko yaliyosongamana.

Amerejelea wito wake wa kuzitaka pande hizo kushirikiana na mwakilishi wake maalum katika kukubali kusitisha uhasama haraka iwezekanavyo na kuanzisha awamu nyingine ya mazungumzo ya amani

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter