Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia iko katika hatihati ya kukabiliwa na tetemeko la haki za binadamu: Zeid

Dunia iko katika hatihati ya kukabiliwa na tetemeko la haki za binadamu: Zeid

Sheria za kimataifa za haki za binadamu zinakiukwa katika migogoro mingi na watu kukwepa mkono wa sheria, huku maelfu ya watu huenda wamekufa na njaa Syria ameonya Jumatatu mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha 31 cha baraza la haki za binadamu mjini Geneva kamishina mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein pia amesema nchini Syria watu 450,000 bado wako katika maeneo yanayozingirwa.

Amegusia pia masuala ya wahamiaji , ak izitaka nchi wanachama kusimama kidete katika suala la chuki dhidi ya wageni ambayo sasa inaenea. Zeid amesema dunia iko katika hatihati ya tetemeko la haki za binadamu, ikighubikwa na ukiukwaji mkubwa katika kila kona.

Akiongeza kuwa licha ya ulinzi wanaopewa watu na sheria za kimataifa za haki za binadamu , bado sheria hizo zinakiukwa kwa kiwango cha kutisha.

(SAUTI YA ZEID)

“Hospitali, vitengo vya matibabu na wafanyakazi wa afya wanpewa ulinzi maalum chini ya sheria za kimataifa za haki za kibinadamu. Lakini hospitali angalau kumi na vitengo vingine vya matibabu vimekuwa vikiharibiwa au kusambaratishwa Syria tangu mwanzo wa mwezi Januari - zaidi ya moja kila wiki - na mara kadhaa shambulio la pili limeathiri shughuli za uokoaji ... Chakula, dawa na msaada mwingine unaohitajika haraka, misaada ya kibinadamu imekabiliwa na vizuizi mara kadhaa. Maelfu huenda wamekufa njaa. "

Naye Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon akizungumza katika kikao hicho amesema ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 ni hatua kubwa kwa ajili ya haki za binadamu..

(SAUTI YA BAN)

“Ajenda inatukumbusha kwamba haki za binadamu zinajumuiosha haki ya maendeleo na kwamba jamii inakuwa imara tuu kama wanachama wake si dhaifu. Ujumuishi, kutogawanyika na asili ya malengo 17 ya maendeleo endelevu chimbuko lake ni haki za kimataifa za binadamu”