Kenya imepiga hatua katika elimu, afya na upatikanaji wa maji safi- Ripoti
Wiki hii, Kenya imewasilisha ripoti yake huko Geneva, Uswisi, kuhusu hali ya haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni mbele ya kikao cha 57 cha kamati ya makubaliano ya kimataifa juu ya haki hizo.
Ripoti hiyo ambayo inaendana na ibara ya 16 ya makubaliano ya kiuchumi, kijamii na utamaduni ICESCR imetanabaisha hatua ambazo Kenya imepiga katika kufanikisha mapendekezo ya makubaliano hayo.
Katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya wa Idhaa hii, mwakilishi wa ujumbe wa Kenya kwenye mkutano huo Dokta. Pasifica Onyancha kutoka wizara ya afya, ameeleza mafanikio yaliyopatikana ambapo hapa anaanza kwa kutaja mambo makuu katika ripoti hio.