Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lapitisha azimio la kusitisha mapigano Syria, majadiliano kuendelea juma lijalo

Baraza la usalama lapitisha azimio la kusitisha mapigano Syria, majadiliano kuendelea juma lijalo

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limepitisha kwa kauli moja  azimio la kuidhinisha ukomeshwaji wa machafuko nchini Syria huku juhudi za mazungumzo ya suluhu la mzozo zikisongeshwa.

Baraza la usalama pia limejdalili hali nchini humo ambapo mwakilishi  maaluma wa Umoja wa Mataifa Syria  Staffan de Mistura amehutubia mkutano huo kwa njia ya video kutoka Geneva.

de Mistura ametaka pande kinzani kutii azimio hilo kwa kusitisha mapigano ilikutoa ahueni kwa raia wanaoendelea kuwa wahanga wa machafuko.  Kadhalika ametangaza kuwa majadiliano yataanza tena juma lijalo.

(SAUTI STAFFAN)

"Iwapo usitishwaji wa mapigano utaendelea kudumishwa kwa mapenzi ya Mungu, na ufikishwaji wa misaada ya kibinadamu utaheshimiwa , natarajia kwa mashauriano na Katibu Mkuu na kwa idhini yenu kuanzisha tena majadiliano kuhusu Syria mnamo Jumatatu ya Machi saba."

Mapema mjini Geneva kikosi kazi cha usaidizi wa kiamataifa kwa Syria ISSG kikiwa chini ya uenyekiti wa Urusi kilikutana kupitia makubalianao ya pande kinzani kuhusu kusitisha mapigano ikiwamo kigezo kilichofikiwa mnamo Februari 22 cha ushiriki katika majadiliano.