Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuzuru Afrika Mashariki kumemfanya msanii Drew Holcomb kuvalia njuga umaskini

Kuzuru Afrika Mashariki kumemfanya msanii Drew Holcomb kuvalia njuga umaskini

Mwanamuziki wa Kimarekani Drew Holcomb, ni mmoja wa wasanii waliopata kushiriki katika mfululizo wa vipindi vya Benki ya Dunia, vya Muziki kwa Maendeleo. Baada ya kuzuru maeneo kadhaa ya Afrika Mashariki, msanii huyo kutoka mji wa Nashville, katika jimbo la Tennessee, Marekani, alitambua kuwa kuna uhaba mkubwa wa huduma za maji safi na huduma za kujisafi, pamoja na matatizo ya lishe duni miongoni mwa watoto. Tangu wakati huo, amekuwa akijihusisha na shughuli za mashirika ya kibinadamu, kama vile One Egg na Blood: Water, ili kusaidia kuleta huduma hizi kwa watu wanaozihitaji zaidi.

Katika Makala hii, Drew Holcomb anatupatia kionjo cha muziki wake, na pia anawahimiza mashabiki wake watimize wajibu wao katika kutokomeza umaskini ifikapo mwaka 2030. Flora Nducha anasimulia...