Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia walindwe, misaada iwafikie wahitaji Sudan Kusini: Kyung-wha Kang

Raia walindwe, misaada iwafikie wahitaji Sudan Kusini: Kyung-wha Kang

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu Kyung-wha Kang, leo amehitimisha zaiara yake ya siku mbili nchini Sudan Kusini akitaka pande kinzani kulinda raia na kuruhusu bila vikwazo ufikishwaji wa misaada ya kibinadamu.

Kiongozi huyo ambaye aliambatana na Katibu Mkuu Ban Ki-moon katika ziara hiyo ambapo walikutana na maafisa wa serikali na kutembelea jamii zilizoathirika kutokana na machafuko.

Bi Kang katika ziara yake hiyo kadhalika amekutana na wadau wa masula ya kibinadamu, wanadiplomasia na kisha kuzuru kambi ya wakimbizi inayolindwa na Umoja wa Mataifa, Malakal ambapo ameshuhudia madhara kufuatia machafuko ya silaha yaluyoripotiwa mnamo Februari 17 na 18.

Amesema amesikitishwa na kile alichokishuhudia Malakal kwani raia walitarajia wako salama kisha wameshambuliwa, kuuwawa,kuathiriwa kisaikolojia na kufurushwa. Ametaka washukiwa wa shambulio hilo wawajibishwe.