Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlinda amani wa Chad aua wenzake wawili huko Mali

Mlinda amani wa Chad aua wenzake wawili huko Mali

Taarifa kutoka mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA zinasema walinda amani wawili wameuawa mapema leo asubuhi kwenye kambi ya Kidali nchini humo. Kwa mujibu wa mkuu wa Radio Mikado ya MINUSMA Olivier Salgado walinda amani hao wamepoteza maisha baada ya kupigwa risasi na mlinda amani mwenzao kutoka Chad ambaye hivi sasa anashikiliwa na polisi.

(SAUTI YA SALGADO)

"Askari mmoja alimfyatulia risasi mwenzake , mwingine alikuwa mhanga wa tukio hilo amekufa pia, na uchunguzi umeanzishwa mara moja ili kubaini mazingira yaliyosababisha tukio hilo na mshukiwa amekamatwa."