Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa muongozo kuhusu dalili, na unyonyeshaji kwa watoto wenye virusi vya Zika

WHO yatoa muongozo kuhusu dalili, na unyonyeshaji kwa watoto wenye virusi vya Zika

Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limechapisha nyaraka tatu zenye miongozo kuhusu mambo matatu katika kukabiliana na virusi vya Zika  ambayo ni tathmini ya watoto wachanga wenye vichwa vidogo, utambuzi na uongozi dhidi ya dalili na unyonyeshaji wa watoto.

Katika machapisho hayo WHO imetahadharisha jamii kuwa watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo hutambulika kutokana na kudumaa katika hatua za ukuaji mathalani uwezo wao wa kiakili, hukumbwa na degedege, na hata ulemavu wa viungo ikwamo kutosikia na kutoona.

Kuhusu utambuzi wa dalili za virusi vya Zika WHO imesema kwamba huanza pale ambapo kinga za mwili hushambulia mifumo ya mishipa ya pemebeni mwa mwili na hili laweza kusababishwa na baadhi ya madhara ikiwano homa ya dengue pamoja na virusi vya Chikunganya.

Shirika hilo la afya ulimwenguni limeeleza katika muongozo wa dalili kuwa n imuhimu wafanyakazi wa sekta ya afya wakafundishwa juu utambuzi wa watu wenye dalili hizo ambazo hutambuliwa kama GBS.

Kuhusu unyonyeshaji, muongozo huo unaainisha kuwa hakuna uthibitisho kuwa virusi vya Zika vyaweza kuambukizwa kwa kitendo hicho na kusisitiza kuwa mtoto anapswa kunyonyshwa kama kawaida na kwa mfululizo kwa miezi sita.

WHO mesisistiza kuwa virusi vya Zika huambukizwa na mbu aina ya Aedes na sio kupitia unyonyeshaji na kutaka usaidizi wa ushauri kwa wanawake wanaozaa watoto wenye vichwa vidogo.