Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki ya Miji Salama na Safi bado ni chagamoto Kenya

Haki ya Miji Salama na Safi bado ni chagamoto Kenya

Haki za Binadamu, ikiwa ni pamoja na haki ya nyumba za kutosha, maji safi na salama na usafi wa mazingira ni miongoni mwa haki zilizomo katika Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Kimataifa wa Uchumi, Jamii na Utamaduni ambazo zimeridhiwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Haki hizi ni wajibu wa nchi na wadau wa kimataifa, haiwezi kuondolewa na zinalindwa kisheria. Katika kipengele nambari 25 kwenye Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu kinahusu nyumba za kutosha . Je nchini Kenya, azimio hilo linafuatwa?, Basi ungana na Joseph Msami katika makala hii kufahamu zaidi.